Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Wampoto

Wampoto ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, Wilaya ya Mbinga. Eneo lao ni mwambao wa ziwa Nyasa (kuanzia Hinga, Mbuli, Ngumbo, Ndingine, Mkili, Yola, Nindai, Tawi, Njambe, Mango, Tumbi, Ngehe na sehemu ndogo ya Puulu na Liuli ambako wamechangamana na Wanyasa).

Wanapakana na Wanyasa (kusini), Wamanda (kaskazini) na Wamatengo (mashariki). Wanahusiana zaidi na majirani wao Wamatengo na Wanyasa.

Lugha yao ni Kimpoto, lugha ya Kibantu ambayo mwaka wa 1977 idadi ya wasemaji wake ilihesabiwa kuwa watu 80,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kimpoto iko katika kundi la N10. [1]

  1. http://sw.negapedia.org/search/?&o=0&c=&q=Wampoto

Previous Page Next Page






Mpoto people English Mpotoj EO Мпото Ukrainian

Responsive image

Responsive image