Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Wamasai

Wamasai
Wanaume wa Kimasai, Kenya, 2005.
Wanawake wa Kimasai,

Wamasai ni kabila la watu wanaopatikana Kenya na Tanzania. Kwa sababu ya mila zao, mavazi tofauti na kuishi karibu na mbuga nyingi za Afrika Mashariki, ni miongoni mwa makabila yanayojulikana zaidi hata nje ya Afrika. [1]

Wao wanazungumza Maa, [1] mojawapo ya lugha za familia ya lugha za Kinilo-Sahara inayohusiana na Kidinka na Kinuer. Kwa sababu ya uhamaji, Wamasai ndio wazungumzaji wa Kiniloti wanaoishi kusini zaidi. Pia wameelimika katika lugha rasmi za Kenya na Tanzania: Kiswahili na Kiingereza.

Utafiti juu ya DNA yao umeonyesha walivyoathiriwa na urithi wa nasaba mbalimbali, hata kutoka nje ya Afrika, lakini hasa wa jamii ya Wakushi wa Afrika Mashariki.

Idadi ya Wamasai wa Kenya ilihesabiwa kuwa 1,189,522 katika sensa ya mwaka 2019 na wale wa Tanzania walikadiriwa kuwa 800.000 katika mwaka 2011 [2]; kwa jumla inakadiriwa kuwa 2,000.000 [1] Makadirio hayo ya Wamasai katika nchi zote mbili huenda ikawa vigumu kuyathibitisha kwa sababu ya umbali wa maeneo ya vijiji vyao vingi, na asili yao ya uhamaji.

Kwa asili walikuwa wafugaji na hivyo walihamahama, na sehemu bado wanaishi maisha ya namna hiyo. Ingawa serikali za Tanzania na Kenya zimeweka mipango kuwahimiza Wamasai kuachana na jadi ya uhamaji ili kuishi maisha ya kisasa, bado wameendelea na desturi hiyo. [3] Wao wanadai haki ya kulisha mifugo katika Hifadhi za Taifa katika nchi zote mbili. Hivi majuzi, Oxfam imedai ni lazima mtindo wa maisha wa Wamasai ukubaliwe kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu hawawezi kulima katika majangwa. [4]

  1. 1.0 1.1 1.2 Wamaasai - Utangulizi Jens Fincke, 2000-2003
  2. ripoti kwa lugha Ethnologue code: mas ethnologue.com, '453, 000 nchini Kenya (1994 I. Larsen BTL) ... 430.000 katika Tanzania (1993) ', Gordon, Raymond G., Jr (ed.), 2005. Ethnologue: Lugha ya Dunia, kumi na tano ya toleo. Dallas, Tex.: SIL International
  3. Mwisho wa Wamaasai. Mohamed Amin, Duncan Willetts, Yohana Eames. 1987. Page 122. Camerapix Publishers International. ISBN 1-874041-32-6
  4. "Maasai 'can fight climate change'". 18 Agosti 2008.

Previous Page Next Page






Masai AF شعب الماساي Arabic شعب الماساى ARZ Masái AST Masailər AZ ماسای‌‌لر AZB Маасайҙар BA Масаі BE Масаі BE-X-OLD Масаи Bulgarian

Responsive image

Responsive image