Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Vipaji vya Roho Mtakatifu

Mchoro mdogo wa Vipaji saba, Walters manuscript W.171 (karne ya 15).

Katika Ukristo vipaji vya Roho Mtakatifu ni misimamo tunayotiwa na Roho Mtakatifu wa kuangaza, kuimarisha na kuzoesha akili na utashi wetu ili kushirikiana naye katika mambo ya utumishi wa Mungu.

Kusudi tujue kweli muundo wa Kiroho unaotuwezesha kuishi kama wana wa Mungu, haitoshi tuyajue maadili. Ni lazima tuzingatie pia vipaji vya Roho Mtakatifu, pasipo kusahau namna mbalimbali za kupata msaada wa Mungu. Vilevile, haitoshi tuwe na maadili yote ya Kimungu na ya kiutu, tunahitaji pia tumiminiwe vipaji vya Roho Mtakatifu ili atuongoze nyuma ya Yesu hadi kwa Baba. “Ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake… Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (Rom 8:9,14).


Previous Page Next Page