Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Plato

Sanamu ya kichwa cha Plato.

Plato (kwa Kigiriki: Πλάτων, Platon; 427 KK - 347 KK) alikuwa kati ya wanafalsafa muhimu zaidi wa Ugiriki ya Kale, akiwa mwanafunzi wa Sokrates na mwalimu wa Aristoteles.

Alibuni mawazo mengi yenye maana hadi leo. Wanafalsafa wa kisasa wamesema ya kwamba falsafa yote inamtegemea Plato.

Aliandika mafundisho yake kwa umbo la majadiliano - yaani watu wawili au zaidi wanajadili mawazo wakikubaliana au kutokubaliana nayo. Kwa njia hiyo Plato alipenda kueleza fikra zake.

Mara nyingi Sokrates ni msemaji mkuu katika majadiliano ya Plato. Huonyeshwa akiwauliza watu juu ya yale wanayoyaamini akiendelea kuuliza maswali kama mawazo yao yanalingana na mantiki. Haieleweki ni kiasi gani Plato alitumia kweli mafundisho ya Sokrates mwenyewe au kama alimtumia zaidi kifasihi kama mhusika akieleza fikra zake Plato kupitia mdomo wa Sokrates wa majadiliano.

Kati ya maandiko muhimu zaidi ya Plato ni "Politeia" yaani "kuhusu dola".


Previous Page Next Page






Plato AF Platon ALS ፕላቶ AM Platón AN Plato ANG प्लेटो ANP أفلاطون Arabic أفلاطون ARY افلاطون ARZ প্লেটো AS

Responsive image

Responsive image