Mto Ruvyironza una mwendo wa km 110 na ni tawimto la mto Ruvuvu ambao tena ni tawimto la Mto Kagera[1].
Kwa kuwa mto huo unaishia nchini Tanzania katika Ziwa Viktoria ambalo linatokwa na mto Naili, baadhi ya wataalamu wanahesabu urefu wa Naili kuanzia chanzo cha mto Ruvyironza nchini Burundi[2][3].
Jina linatokana na Mlima Luvironza, mkubwa kuliko yote ya Burundi, ambapo mto una chanzo chake. Mlima Luvironza una kimo cha mita 2,700 juu ya UB na uko kilomita 45 upande wa mashariki wa Ziwa Tanganyika.
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help)