Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Mchanga

Maji na mchanga mwambaoni

Mchanga ni punje ndogo za mwamba uliosagika.

Kufuatana na mapatano ya kitaalamu mawe huitwa "mchanga" kama punje zake ziko kati ya milimita 0.063 hadi 2.

Punje hizo zinatokana na mmomonyoko wa mawe makubwa zaidi kama changarawe yaliyosukumwa na upepo au maji kwa mfano mtoni, baharini au kwenye mteremko wa mlima.

Jina mchanga halitaji mata yake lakini mara nyingi inamaanisha punje za silika (Si02) ambayo ni oksidi ya silikoni inayopatikana kwa wingi katika ganda la Dunia.

Mchanga hupatikana kwa wingi hasa kando ya bahari, jangwani au mtoni.

Mchanga ukichanganywa na saruji na maji huwa zege inayotumiwa kwa ujenzi.

Mchanga wa silika inaweza kuyeyushwa kuanzia jotoridi ya sentigredi 1713 na hivyo ni msingi wa kutengeneza kioo.


Previous Page Next Page






Sand AF Arena AN Sand ANG رمل Arabic ܚܠܐ (ܕܚܝܚܐ) ARC رملة ARY বালি AS Sable (material) AST Aqu AY Qum (süxur) AZ

Responsive image

Responsive image