Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Jumamosi kuu

Sanamu maarufu ya Pietà ya Michelangelo iliyochongwa katika marumaru kumuonyesha Bikira Maria akipakata maiti ya mwanae Yesu mara baada ya kifo chake msalabani.
Picha takatifu ya Jumamosi Kuu na Takatifu, ikimuonyesha Yesu Kushukia kuzimu.

Jumamosi kuu ni siku ya Juma kuu inayoadhimisha hasa pumziko la mwili wa Yesu Kristo kaburini na roho yake kushukia kuzimu kabla ya kufufuka kwa utukufu usiku wa kuamkia Jumapili ya Pasaka.

Tarehe yake inabadilikabadilika kila mwaka na hata mwaka uleule ni tofauti katika madhehebu ya Ukristo, hasa yanayofuata mapokeo ya mashariki na yale yanayofuata mapokeo ya magharibi.

Siku hiyo Misa na sakramenti mbalimbali haziadhimishwi kwa kuwa wafuasi wa Yesu wanatulia kimya wakitafakari matukio ya Ijumaa kuu na kujiandaa washangilie ufufuko wake kuanzia kesha la Pasaka hadi Jumapili ya Pentekoste siku 50 baadaye.


Previous Page Next Page