Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Wamanyema

Kijiji cha Wamanyema 1876

Wamanyema (Una-Ma-Nyema, yaani Wala-samaki), ni jamii ya vikabila na koo zisizopungua 18 ya Kibantu yenye asili ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mkoa wa Kigoma nchini Tanzania hasa wilaya ya Kigoma katika manispaa ya Kigoma-Ujiji.

Manyema Association imeundwa miaka ya 1930, Wamanyema waliunganishwa na utamaduni wa kiswahili - kiruwa, imani ya dini ya Kiislamu na asili ya mashariki ya Kongo.

Kwa Tanzania, wanajumuisha makabila ya Wagoma, Wabwari, Wakusu, Waholoholo n.k. ambao wote huitwa Wamanyema.

Kwa sehemu kubwa ya karne ya 19 waliwindwa sana na Waarabu waliofanya biashara ya watumwa.

Wamanyema walipofika Kigoma kuna ambao walipata majina katika miji kama Katonga, Kabwe, Mkabogo au Kabogo: hao wote walikuwa Wamanyema wenye asili ya Kongo.

Wamanyema shughuli yao kuu ni Uvuvi na Biashara na hupendelea zaidi kuishi kifamilia.

Hivyo Wamanyema na Waha ndio wenyeji wa Kigoma. Uenyeji huu tunaouzungumza ni miaka ya zamani sana: hata kabla ya kuanza kwa ukoloni hawa watu tayari walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa wakipendana na kuthaminiana. Kuna vitu Waha waliwafundisha Wamanyema na pia kuna vitu Wamanyema waliwafundisha Waha na wote hawa waliipigania Tanganyika kutoka mikononi mwa serikali ya kikoloni. Hata mradi wa kuligawa bara la Afrika kati ya nchi kadhaa za Ulaya ulikuwa bado kabisa Wamanyema na Waha walikuwa wakiishi pamoja.


Previous Page Next Page






Manyema English Manyema Spanish Manyema HA Maniemas Portuguese

Responsive image

Responsive image